Diamond Platinumz atakuwa ni msanii pekee wa Tanzania atakayeungana na wasanii walio kwenye orodha A, katika kuhudhuria utoaji wa tuzo za Africa Music Magazine(Afrimma) zitakazofanyika Jumamosi July 26,Eisemann Center,Texas nchini Marekani.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na African Muzik Magazine na Big A Entertainment zimelenga hasa katika kuwatunuku wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika waliopo duniani kote na itagusa nyanja mbalimbali za burudani.
Bright Okpocha aka Basket Mouth ambaye mchekeshaji maarufu wa Nigeria na mrembo wa Nollywood Juliet Ibrahim (Ghana) watakuwa washereheshaji wa tuzo hizo.
0 comments:
Post a Comment