Albert Mangwea ni miongoni mwa wasanii wanaoaminika kuwa na nyimbo nyingi sana ambazo bado hazijatoka,wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Mangwea Morogoro iliyofanyika November 2013 Millardayo.com iliongea na familia yake kuhusu mpango wa nyimbo ambazo bado hazijatoka za Mangwea.
Keneth Mangwea kaka wa Marehemu Mangwea alisema wanashirikiana na rafiki wa karibu wa Marehemu Mangwea M to The P kukusanya nyimbo kwenye studio tofauti tofauti ambazo aliwahi fanya marehemu Mangwea na nia ni kuziweka kwenye album moja.
Leo kupitia XXL ya Clouds Fm Mama mzazi wa Mangwea ameomba kwa watayarishaji wote[Producers]ambao Marehemu Mangwea amewahi kufanya nao kazi kumletea nyimbo hizo kwa ajili ya kupata haki miliki[Copyright]Mama mzazi katoa namba za simu ili ikitokea ukiamini unao hata wimbo mmoja wa Marehemu umpigie.
Namba hizo alizozitoa mama ni 0754 967738,0755 303552 na 0718 592620 hii ni kama una kazi za Marehemu Mangwea.
source @ www.millardayo.com
0 comments:
Post a Comment