sammisago.com imepiga story na G- Warawara kutaka kufahamu sababu zilizompelekea kuchukua uamuzi huo.
“Yaani sasa hivi muziki umekuwa ni kazi vilevile ni biashara. Kwa hiyo biashara ni mimi mwenyewe, yaani mimi mwenyewe ni biashara. Kwa hiyo nikifanya kazi na wewe ni kama nimechukua biashara yangu nimeileta kwako. Kwa hiyo tunauza bidhaa. Tukijumlisha pamoja tunakuwa tunauza bidhaa. Kwa hiyo tunapotaka kuuza bidhaa lazima faida ipatikane sehemu zote mbili. Hilo ndilo lengo kubwa.”
Akielezea mfumo wa bei aliojiwekea, G-Nako amesema bei yake haitofautiani sana kati ya msanii mkubwa na msanii mdogo, ni makubaliano ya kawaida tu anayofanya bila kujali.
Amesisitiza kuwa kigezo kikubwa kwake ni wimbo mzuri na kuhakikisha inatoka kazi nzuri siku zote kabla ya kupanga malipo.
“Pamoja na yote hayo lazima tutengeneze muziki mzuri. Kwa hiyo mimi kitu kikiwa kwenye feeling zangu mara nyingi huwa nakifanya nikiona kitu kinataka kuwa kizuri mara nyingi huwa nakifanya. Ni kama ambavyo kuwa nakuambia siku zote mnapokutana wasanii wawili wazuri lazima mtatengeneza kitu kizuri.”
credit: sammisago.com
0 comments:
Post a Comment