AY kwenda Miami kushoot video ya ‘It’s Going Down’

Rapper Ambwene Yesaya aka AY amesema atasafiri hadi jijini Miami nchini Marekani kwenda kushoot video ya wimbo wake mpya ‘It’s Going Down’ aliomshirikisha msanii wa Uingereza Ms Trinity na Mmarekani, Lamyia Good.
AY amesema ameamua kwenda kufanya video jijini Miami na sio kushoot Tanzania ili kupunguza gharama ya kuwaleta wasanii hao. “Nimefanya hivyo ili kuepusha baadhi ya gharama kwasababu ukisema wao waje huku, Trinity huwa hasafiri peke yake, Lamyia hasafiri peke yake, hapo unaweza kushangaa unalipa tiketi hata sita wakati mimi nikienda kule naenda peke yangu nafanya accommodation mimi,” amesema AY kwenye mahojiano na kipindi cha Daladala Beat cha Magic FM
AY amedai kuwa ni rahisi pia kufanya video Marekani kwakuwa meneja wake wa kimataifa anaishi huko huko. Amesema video ya wimbo huo itatoka mwezi ujao na amepanga kwenda Marekani kushoot wiki ijayo.
“Kushoot video Miami kutaleta maana kutokana na mazingira ya kule, location na hali ya hewa inaweza kuleta picha nzuri,” ameongeza.
Share on Google Plus

About IF YOU DON'T KNOW NOW YOU KNOW

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment