#NEWS : "QUEEN DARLEEN NA SUMA LEE NDIO WALIOGUNDA KIPAJI CHANGU" ASEMA BELLE 9.

Msanii wa Morogoro, Belle 9 amesema Suma Lee na Queen Darleen ndio waliogundua kipaji chake kipindi wasanii hao walipoenda mkoani Morogoro kwenye show wakati huo akiwa bado underground.

Belle amesema alifanya show kabla ya wasanii hao kupanda na ndipo Suma Lee alipomwambia promota aitwaye Bonga kuwa ‘dogo anaweza mchukue’. Baada ya hapo anasema ‘nilienda kupiga picha na Suma Lee na Queen Darleen, hiyo picha hadi leo ninayo. Nakumbuka wali ninunulia na soda wakaniambia ‘dogo unaweza sana’ ndipo baadaye nikachukua namba za Bonga ndo nikaja Dar nikarekodi kwenye studio za G Records producer alikuwa KGT,” Belle 9 

“Nakumbuka nilirekodi chorus tu, nilikaa tu Dar baadaye nikwambia Bonga kwakuwa yeye ndo alinileta Dar, nikamwambia ‘ngoja mie nirudi tu home Moro’ hapo akanimbia ‘sawa basi hamna shida nitafanya mpango basi uipate ile beat’. Akanimbia atafanya mpango nipate ile beat niandikie. Hizo ndo moja ya husstle nilizopitia kabla sijatoka. Huwa wananikumbuka hadi leo nawasiliana nao.”
Share on Google Plus

About IF YOU DON'T KNOW NOW YOU KNOW

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment