#NEWS : "SINA MPANGO KUFANYA COLLABO NA ALI KIBA" ASEMA SHETA

Shetta ni msanii ambaye karibia nyimbo zake zote alizotoa amewashirikisha wasanii mbalimbali wa nyumbani. Alimshirikisha Belle 9 kwenye ‘Nimechokwa’, Rich Mavoko kwenye ‘Sina Imani’, Dully Sykes na Tunda ‘Mdananda’, Linah kwenye ‘Bonge la bwana’ na amemshirikisha Diamond katika nyimbo mbili ‘Nidanganye’ na ‘Kerewa’.

Sheta ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaofanya kazi na hit makers wa bongo kwenye nyimbo zake amezungumzia uwezekano wa collabo na Ali Kiba

Swali> Sheta Unampango wa kufanya wimbo wa Ali Kiba 

Jibu [Sheta]> Sina mpango wa kufanya kazi Na Ali Kiba, Hizo Habari umetoa wapi, Kwa sasa sina mpango wa kufanya wimbo na msanii wa nyumbani, naangalia International au nifanye wimbo mwenyewe, 
Swali> Tungependa kujua wasanii wa nje unaopanga kufanya nao kazi 
Jibu [Sheta]> Wako kama watano, uongozi unaangali yupi anafaa na atapatikana, siku tayari kusema majina sasa ila wimbo uko tayari. 
Share on Google Plus

About IF YOU DON'T KNOW NOW YOU KNOW

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment