Akihojiwa kwenye kipindi cha Ladha 3600 cha EFM,Darassa amedai kuwa ndoto zake za kimuziki zimemfanya awe anafanya kazi muda mwingi zaidi hivyo kukosa muda wa kukaa na watu watu wake wa karibu kama ilivyokuwa zamani.
“..sasa hivi nimekuwa na wakati mgumu hata na baby,wakati mgumu na ndugu zangu pamoja na washikaji, hatuonani mara nyingi sana..hatupigi sana stori kwa sababu kuna goli nalihangaikia,so once nikiwa poa itakuwa ni rahisi kufanya vitu vingine,ila kuna vitu nahitaji kufanya kwa sasa” alifunguka Darassa na kuwataka mashabiki zake wategemee ngoma kali zaidi kutoka kwake.
0 comments:
Post a Comment