Ni kwasababu katika kipindi cha miaka miwili, Joh amefanikiwa kuachia ngoma zilizofanya vizuri kwenye vituo vya redio na runinga nje na ndani ya Tanzania. Hata hivyo, Joh anasema kukosa nomination za tuzo hizo mwaka huu, hakuwezi kumpunguzia kitu.
“Katika muziki wangu huwa sifikirii kuhusu tuzo,” Joh alimweleza mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Hivyo ni vitu tu ambavyo vinakuja baadaye. Kupata au kukosa, au kutokuwa nominated kwenye tuzo aina yoyote ile kwangu haimaanishi kwamba nimenyang’anywa kitu katika uwezo ambao mwenyezi Mungu amenipatia,’ alisema Joh Makini.
‘Hiyo kwangu ni kawaida sana na wala haiwezi kutia doa kwenye brand ya Joh Makini.’
0 comments:
Post a Comment