#NEWSMASHARIKI: Wyre kurudia kazi za Kanda Bongoman

Wyre, staa wa muziki kutoka nchini Kenya amefanikiwa kupata haki ya kufanyia kazi upya ya nyimbo kali kabisa kabisa za msanii mkongwe wa Muziki wa kiafrika, Kanda Bongoman.


Kanda Bongo Man na Wyre
Kupitia nafasi hii, Wyre anatarajiwa kutoka na kazi ambayo imeboreshwa na ina vionjo vya kisasa kutoka rekodi kama Inde Monie ambayo iliweza kutikisa mawimbi vilivyo katika kipindi cha nyuma.
Wyre amekuwa na rekodi ya kuzitendea haki ngoma za zamani ambazo anazirudia, kitu ambacho kinawapatia mashabiki hamu kubwa zaidi kuona kile atakachofanya kutoka kazi za Kanda Bongoman.
Share on Google Plus

About IF YOU DON'T KNOW NOW YOU KNOW

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment