#News : Kanye West amuomba Msaada Boss wa Facebook

Mwanamuziki Kanye West amemuomba hadharani mwaanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg ampe usaidizi wa kifedha. West anataka Zuckerberg awekeze $1bn (£700m) katika miradi yake akisema yeye binafsi hana “rasilimali za kutosha” kuunda kile ambacho “anaweza”.

Ametoa ombi hilo siku chache tu baada ya kutangaza kwamba ana deni la $53m (£36m) alipokuwa akitoa albamu yake mpya. West alijitetea kupitia msururu wa jumbe kwenye Twitter.

Waandishi wa BBC Newsbeat wamewasiliana na maafisa wa Facebook ambao wamesema: “Hatuna lolote la kusema kwa sasa.” Jambo la kushangaza ni kwamba Kanye West amemuomba Zuckerberg usaidizi kupitia Twitter ambao ni mtandao unaoshindana na Facebook.


Share on Google Plus

About IF YOU DON'T KNOW NOW YOU KNOW

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment