Kupitia kipindi Cha Planet Bongo cha East Africa Radio ambapo Chid benz alipewa "Heshima ya bongo fleva" alifunguka na kusema wakati wapo Mj Records kufanya kazi hiyo Ali Kiba alidondosha chozi sababu yeye alimfungia mlango ndani na kumwambia hawezi kutoka mpaka atakapo maliza kuweka vocal.
AliKiba
"Unajua mdogo wangu Ali Kiba alipoingia booth mimi nikamfungia mlango kabisa ili asitoke so akawa analalamika maana mle ndani kulikuwa na joto sana, lakini nikamwambia mdogo wangu huwezi kutoka mpaka umalize kazi baada ya hapo akalia kisha akakaa zake chini baadae aliinuka na kuendelea na kazi mpaka mzigo ulipoisha ndio nikamfungulia mlango na kutoka " Amesema Chid Benz
Katika hatua nyingine Chid Benz amesema licha ya yeye kufanya muziki wa Hip hop lakini alikuwa na mashabiki wengi wakike kutokana na sauti yake pamoja aina ya nyimbo alizokuwa akiimba.
"Unajua kwangu mimi niliweza kuwa na mashabiki wa kike wengi kutokan na ukweli kwamba wanawake wanapenda sana sauti nzuri na nzito na mimi Mungu amenijalia sauti lakini pia nilikuwa naimba sana mapenzi lakini napochana kwenye mapenzi nilikuwa sifanyi zile ngumu lakini kingine nilikuwa naweza kuyaelezea vizuri mapenzi" Aliongeza Chid Benz
0 comments:
Post a Comment