Akizungumza kwenye Friday Night Live show inayorushwa saa tatu usiku na EATV na EA Radio baada ya kuulizwa kwanini hakuonekana kwenye video hiyo wakati ilikuwa ni moja ya video kubwa kwa AY aliyo itoka kwa wapendanao.
Dela ameeleza sababu ya kutokuwepo kwenye video hiyo nikutokana na ratiba yake kuingiliana na ratiba ya uandaaji wa video hiyo kwakuwa hakuwepo njchini Kenya wakati AY alikuwa nchini humo, lakini yeye na AY hawana tofauti yoyote bali ni marafiki wazuri.
Dela pia ambaye amefanya cover ya wimbo wa Adele 'Hello', ameeleza kuwa kufanya cover ya wimbo flani sio kutafuta kick au kujipendekeza kwa msani huyo bali nikuonyesha uwezo wako kwenye kuimba. Kwasasa Dela anajipanga kufanya cover ya wimbo wa hotline bling wa rapper Drake huku akizidi ku hit kwenye wimbo na video yake ya Third Party Lover.
0 comments:
Post a Comment