#NEWS: Raymond: Nilikata tamaa na sikua naamini kutoka kimuziki

Raymond (Rayvan) akiwa na Diamond Platnumz
Maisha ni safari ndefu yenye vikwazo vingi lakini hatutakiwi kukata tamaa kwa kuwa huwezi kujua kesho yako. Raymond aliwahi kukata tamaa kwenye muziki wake lakini alijitahidi hatimaye amekuwa ni mmoja kati ya wasanii hatari na wenye kutazamwa kwa jicho la ziada.
Muimbaji huyo wa WCB amemshukuru bosi wake Diamond kwa mchango wake pamoja na kumuamini kwa kumshirikisha kwenye wimbo wa Salome ambao umekuwa gumzo mitaani kwa sasa.
Kupitia mtandao wa Instagram, Raymond ameandika “Mengi yako Moyoni Mwangu.lakini kiukweli siamini hapa nilipo.nilikata tamaa,sikujiamini tena kama ntaweza kufika.kuna muda nilijiona sina bahati hadi nikaanza kuichukia sauti yangu.lakini wewe ulinishika mkono nakunionyesha njia mengi umenielekeza haukuishia hapo ukaona unipe nafasi tufanye kazi moja mimi na wewe #SALOME . Am so proud of you @diamondplatnumz #SALOME

Share on Google Plus

About IF YOU DON'T KNOW NOW YOU KNOW

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment