#NEWS: 'Shika adabu yako' ilitakiwa kuwa video chafu sana, asema Director wa video hiyo Nicklass

Aliye iandaa video ya Shika Adabu Yako" yakwake Nay wa Mitego, Director Nicklass amesema kuwa video hiyo ilikuwa iwe chafu zaidi kutokana na kuwa nay wa Mitego alisha ona wimbo huo umeshafungiwa kuchezwa kwenye radio za hapa nchini hivyo basi na video haitaweza kupata air time.
Amezungumza hayo kwenye Friday Night Live ya East Africa TV na East Africa Radio show inayoruka saa tatu usiku kwenye channel hiyo ambapo alisema mabadiliko ya kutoweka fanya video hiyo kuwa chafu yalikuja baada ya baadhi ya runinga kuwasilianan na Nay kumuomba awapelekee video hiyo ikisha kamilika ili waicheze.

Nicklass alipoulizwa kuhusiana na scene inayojulikana imemlenga mwanamuziki Shetta kuhusiana na umiliki wa gari lake la kifahari, Director huyo alisema kuwa "...Scene hiyo Nay ndiyo aliichaguwa iwepo lakini hata wakati inaandaliwa hakuwepo kutokana na kuiogopa...".

Wimbo wa Shikia adabu yako wa Nay wa Mitego ulipata air time fupi sana pale tu ulipotoka kwenye vituo baadhi vya radio na kisha BASATA kutolewa tamko kuwa wimbo huo hauna maadili na haufai kusikilizwa.
Share on Google Plus

About IF YOU DON'T KNOW NOW YOU KNOW

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment